Story by Hussein Mdune-
Kuna haja ya wanawake kuwa mstari wa mbele kuwapigia debe wanawake wenzao ambao wanawania nyadhfa mbalimbali za uongozi wakati wa uchaguzi huu wa Agosti 9.
Haya ni kulingana na Mshirikishi wa chama cha UDM kanda ya pwani Nuria Huka aliyesema tabia ya wanawake kudharauliana hasa katika masuala ya uongozi kumechangia wengi wao kusalia nyuma kimaendeleo.
Nuria amewataka wagombea wa kiume kuwaunga mkono wanawake ambao wamejitokeza kuwania nyadhfa za uongozi, akihoji kwamba hatua hiyo itabadili taswira ya uongozi nchini
Hata hivyo amewataka wanawake kutokubali kutumiwa vibaya na wanasiasa na badala yake kudumisha amani.