Story by Bakari Ali –
Wanawake wamehimizwa kujitokeza na kuwania nyadhfa mbalimbali za uongozi ili kuhakikisha wanapata uwakilishi sawa serikalini na kushirikishwa katika masuala ya maendeleo.
Akizungumza katika kongamano la 3 la wanawake mjini Mombasa, Katibu mkuu msimamizi katika idara ya jinsia Dkt Linah Jebii Kilimo amesema kuna umuhimu mkubwa wa wanawake kujitokeza na kuwania nyadhfa za uongozi.
Dkt Linah amepongeza hatua ya viongozi wa kike katika taasisi na idara mbalimbali nchini kwa juhudi walizoweka katika kazi zao licha ya changamoto mbalimbali wanazozikumba katika utendakazi wao.
Akiunga mkono kauli hiyo, Mwenyekiti wa taasisi ya usimamizi wa raslimali nchini Joseph Onyango amewahimiza wanawake walio na ari ya kuwania nyadhfa za uongozi kutohofia lolote na badala yake kujitosa katika ulingo wa siasa.