Story by Mercy Tumaini –
Wanawake wenye nia ya kuwania nyadhfa mbalimbali za uongozi katika kaunti ya Kilifi wakati wa uchaguzi mkuu ujao wameshauriwa kutoogopa lolote na badala yake kujitosa katika kinyang’anyiro cha kisiasa.
Wanaharakati wa maendeleo katika eneo bunge la Rabai Esther Kondo amesema idadi kubwa ya wanawake katika eneo bunge la Rabai wamekuwa wakiogopa masuala ya siasa kutokana na mila na Tamaduni ambazo zimekuwa zikiwadunisha.
Akizungumza katika bunge la Rabai, Esther amesema huu ndio wakati mwafaka kwa wanawake kuonyesha uwezo wao wa kubadili uongozi wa duni unaoshuhudiwa nchini.
Wakati uo huo amesema kutokana na changamoto zinazowakumba wanawake hasa ukosefu wa maji safi, miundo msingi miongoni mwa masuala mengine muhimu, kuna haja ya wanawake kuungana na kubadili uongozi duni.