Wanawake wafuasi wa dini ya Kiislamu wametakiwa kutosalia nyuma na kujitokeza kupigania nafasi mbalimbali za uongozi ikiwemo katika mahakama za Kadhi nchini.
Mwanaharakati wa kijamii kaunti ya Mombasa Mesaidi Omar amesema wanawake wa jamii hiyo hawastahili kusalia nyuma bali kuziwania nyadhfa mbalimbali za uongozi.
Akizungumza katika kaunti ya Mombasao, Msimamizi huyo mkuu wa miradi katika Shirika la Haki Afrika amesema uteuzi wa Jaji mkuu nchini Martha Koome ni ishara kamili kwamba wanawake wana uwezo wa kuongoza nchi.
Hata hivyo amesisitiza kwamba ni sharti mswada wa thuluthi mbili ya usawa wa kijinsia upitishwe bungeni na kuwa sheria ili kutoa nafasi kwa wanawake katika uongozi.