Picha kwa hisani –
Viongozi wa kike katika kaunti ya Kilifi wamejitokeza na kuweka wazi kwamba hawatoruhusu wanasiasa wa kaunti hio kuendeleza siasa za matusi ambazo huenda zikaliweka taifa pabaya.
Wakiongozwa na mwakilishi wa kike kaunti hio Bi Getrude Mbeyu viongozi hao wamesema wamechoshwa na hatua ya baadhi viongozi wa Kilifi kuwatusi viongozi wakuu serikalini.
Kwa upande wake seneta mteule Christine Zawadi amesema siasa za mapema zinazoendelezwa na viongozi wa humu nchini zimechangia pakubwa siasa za matusi na mgawanyiko.