Mkurugenzi mkuu wa Shirika linaloangazia maslahi ya wahanga wa biashara haramu ya ulanguzi wa binadamu la ‘Trace Kenya’ Paul Adhoch amesema wanawake katika eneo la Pwani wamo katika hatari ya kujipata kwenye mtego wa walanguzi wa binadamu.
Adhoch amesema Wanawake wamekuwa wakihadaiwa kwa urahisi na kisha baadaye kujipata katika njia panda hasa mikononi mwa walanguzi wa binadamu.
Akizungumza mjini Mombasa, Adhoch amesema ni lazima wakaazi wa Ukanda wa Pwani wahamasishwe kuhusu athari za biashara haramu ya ulanguzi wa binadamu.
Wakati uo huo amedokeza kuwa sio rahisi kwa washauri kuwabadili kifikra wale wanaopitia mikononi mwa walanguzi, akisema wengi wao hukanganywa akili na kushindwa kurudi makwao.
Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.