Story by Ephie Harusi –
Mwenyekiliti wa Shirika la kijamii la Kilifi Mums Kibibi Ali amewataka wanaume wanaopitia dhulma za kijinsia katika kaunti ya Kilifi kujitokeza na kuzungumza ili waweze kupata usaidizi.
Kulingana na Kibibi, hali ya wanaume kuwa na msongo wa mawazo imechangia wengi wao kujihusisha katika visa vya mauaji hasa kwa jamaa wao wa karibu.
Akizungumza na Wanahabari, Kibibi amesema ni wanawake pekee ambao wamekuwa wakijitokeza na kuzungumzia visa hivyo pindi wanapodhulumiwa huku wanaume wameonekana kusalia kimya.
Wakati uo huo amesema kwa sasa wanawake katika kaunti ya Kilifi wanafahamu haki zao kufuatia hamasa ambazo wamekuwa wakipokea kutoka kwa mashirika ya kijamii.