Story by Bakari Ali–
Mgombea wa kiti cha ubunge wa Mvita kupitia chama cha UDA Omar Shallo na mgombea wa uwakilishi wadi ya Tudor Samir Baloo wamekamatwa na polisi.
Wawili hao wametiwa nguvuni baada ya kuzua sintofahumu za kisiasa katika kituo cha kupigia kura cha Marycliff eneo bunge la Mvita.
Wawili hao wanazuiliwa na polisi katika kituo cha polisi cha Makupa kaunti ya Mombasa.
Maafisa wa polisi wamesema viongozi hao wawili wanahojiwa kuhusiana na vurugu hizo na huenda wakafikishwa Mahakamani kujibu mashtaka ya kuzua rabsha katika vituo vya kupigia kura.