Story by Our Correspondent–
Mgombea wa kiti cha ugavana katika kaunti ya Kilifi kupitia chama cha PAA, Wakili George Kithi amesisitiza kwamba kuna haja ya zoezi la kura ya mchujo katika vyama mbalimbali vya kisiasa nchini kuzingatia haki na usawa.
Akizungumza katika kaunti ya Kilifi wakati wa mikutano yake ya kisiasa, Kithi amesema kuna haja ya wasimamizi wakuu wa vyama vya kisiasa kutumia ratiba ya sajili ya wapiga kura ili kuhakikisha wananchi wanachagua viongozi waadilifu.
Kiongozi huyo amesema iwapo vyama vya kisiasa vitazingatia haki, usawa na demokrasia basi zoezi la kura ya mchujo nchini litashuhudia haki na uwazi sawa na kufanikisha uchaguzi mkuu wa amani.
Wakati uo huo amewarai wakaazi wa kaunti ya Kilifi na viongozi wa kisiasa kujitenga na siasa za vurugu na malumbano, akisema taifa hili linahitaji amani huku akiwaria wakaazi wa kaunti hiyo kuunga mkono azma yake ya kuwania kiti cha ugavana kaunti ya Kilifi.