Story by Gabriel Mwaganjoni-
Viongozi wa dini ya Kiislamu katika kaunti ya Mombasa wamewatahadharisha viongozi wa kisiasa dhidi ya kuwachochea wananchi kufarakana.
Wakiongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la mashauri ya kiislamu nchini KEMNAC Sheikh Junga Ngao, viongozi hao wamekariri kwamba katika siku za hivi majuzi kumekuwa na utata na malumbano makali miongoni mwa wanasiasa na wafuasi wao.
Kauli yake imeungwa mkono na Mufti mkuu humu nchini Sheikh Juma Omar aliyehoji kwamba ni sharti swala la amani katika kampeni za kisiasa lizingatiwe.
Wakati uo huo, aliyekuwa Kamishna wa Wakfu unaosimamia mali ya waislimu nchini Zuber Noor amewataka wananchi kuwachagua viongozi watakaobadili hali ngumu ya maisha inayolikumba taifa hili kwa sasa.