Story by Ali Chete-
Naibu wa msajili wa vyama vya kisiasa nchini Florence Birya amesema hakuna chama cha kisiasa kitakachosajiliwa kwa misingi ya kikabila, kimaeneo ama kidini.
Akizungumza na Wanahabari katika kaunti ya Mombasa, Florence amesema vyama vyote vya kisiasa nchini ni lazima vitimize kanuni za Katiba kuhusu vyama vya kisiasa ndio viweze kusajiliwa na wala sio kwa misingi ya kidini ama kikabila.
Florence amesema vyama vyote vya kisiasa ni lazima viwe na sura ya nchi, akihoji kwamba iwapo viongozi wa kisiasa watalizingatia shinikizo hilo basi taifa hili litashuhudia amani.
Wakati uo huo amewataka wakenya kutembelea mtandao wa e-citizen ili kujua vyama ambavyo wamejisajili kisheria.