Picha kwa hisani –
Viongozi wa kisiasa katika kaunti ya Lamu wametakiwa kuzingatia kanuni za kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona wanapofanya mikutano yao ya kisiasa.
Kamishna wa kaunti ya Lamu Irungu Macharia amesema wanasiasa wanapaswa kuandaa mikutano yao katika kumbi zilizoko mijini ili kudhibiti idadi ya watu watakaohudhuria mikutano hiyo na wala sio kufanya mikutano hiyo viwanjani.
Macharia amesema ni lazima wanasiasa kuhakikisha watu wanaohudhuria mikutano hiyo ya kisiasa wanazingatia kanuni za Wizara ya Afya nchini za kudhibiti Corona hasa kwa kuvaa barakoa na kukaa umbali wa mita moja.
Wakati uo huo amewataka wanasiasa kutoa taarifa kwa idara ya usalama kabla ya kuandaa mikutano yao ya kisiasa ili kuhakikisha usalama wao unalindwa.