Story by Gabriel Mwaganjoni –
Wanasiasa humu nchini wametakiwa kukoma kuikashfu idara ya mahakama kuhusu swala la kuifanyia marekebisho katiba kupitia mchakato wa BBI.
Mwenyekiti wa Shirika linalopigania maswala ya Amani na uiano la Kenya Peace Agenda Forum Kasisi Francis Kanja amesema wakenya hawapaswi kulazimishiwa mchakato wa BBI na uamuzi wa mahakama unapaswa kuheshimiwa.
Kanja aliyekuwa akizungumza katika eneo la Bamburi kaunti ya Mombasa amesema ni wazi wanasiasa wana malengo fiche kuhusu swala la BBI akiwataka wakenya kujitenga na swala hilo na kuheshimu uamuzi wa mahakama.
Hata hivyo amewataka wakenya na hasa wakaazi wa eneo la Pwani kutogawanywa na mchakato wa BBI wala wanasiasa mashinani na badala yake kukumbatia mshikamano na kudumisha amani.