Picha kwa hisani –
Viongozi wa kisiasa wanaoegemea upande wa naibu wa rais William Ruto wamejitokeza na kukashifu uongozi wa gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho.
Wakiongozwa na aliyekua seneta wa Mombasa Hassan Omar Sarai na mbunge wa Malindi Aisha Jumwa, viongozi hao wamesema gavana Joho hana nia yeyote ya kuleta mabadiliko katika ukanda wa pwani.
Kwa upande wake mbunge wa Kilifi kaskazini Owen Baya ameweka wazi kwamba chama cha kisiasa cha pwani kitazinduliwa rasmi hivi karibuni na kupitia muungano huo watafanikisha maendeleo ya ukanda huu.