Story by Gabriel Mwaganjoni-
Mgombea wa kiti cha ubunge wa Changamwe Munywoki Kyallo amesema Wanasiasa katika kaunti ya Mombasa wana jukumu kubwa la kuhakikisha mikutano yao ya kisiasa haishuhudii vurugu.
Kyallo amesema vurugu za mara kwa mara zinazoikumba mikutano ya kisiasa mara nyingi huchangiwa na wanasiasa wenyewe kutokana na tamaa zao za uongozi.
Akizungumza katika eneo la Changamwe, Kyallo amesema ni sharti swala la vurugu za kisiasa likomeshwe mara moja huku akiwataka wanasiasa kukumbatia siasa za amani na kuuza sera zao kwa uadilifu.
Wakati uo huo, amewataka wanasiasa kujitenga na siasa za chuki na ukabilia akilitaja tukio la hivi majuzi la kupigwa risasi kwa mgombea wa ubunge wa Mvita Ali Mwatsahu kama lisilofaa.