Story by Hussein Mdune-
Mgombea wa kiti cha useneta kaunti ya Kwale Antony Yama amewataka viongozi wa kisiasa kujitenga na siasa za ukabila na vurugu na badala yake kuhubiri amani.
Akizungumza katika mikutano yake ya kisiasa, Yama amesema siasa za ukabila hazina malengo ya maendeleo na kuwasisitiza wakaazi kuwa makini dhidi ya viongozi wenye tabia hizo.
Yama hata hivyo amewapongeza viongozi wa chama cha UDA kwa kumpatia tiketi ya moja kwa moja ya chama hicho ili kuwania kiti cha useneta kaunti ya Kwale.
Yama ambaye pia ni Mwakilishi wa wadi ya Kasemeni amewataka wakaazi kaunti ya Kwale kuwachagua viongozi kwa kuzingatia sera za maendeleo.