Story by Rasi Mangale
Viongozi wa kisiasa humu nchini wamehimizwa kutowagawanya wakenya kwa misingi ya kisiasa wakati huu ambapo wananchi wanajiandaa kwa uchaguzi mkuu
Mjumbe maalum katika bunge la kaunti ya Kwale Najma Mwandoto, amewahimiza wanasiasa kufanya kampeni za amani sawa na kuwaunganisha wananchi katika msingi ya uwiano.
Akizungumza na Wanahabari, Najma amesema iwapo wanasiasa wengi watafanya kazi pamoja sawa na kushirikiana na wananchi basi taifa hili litazidi kushuhudia amani hata baada ya uchaguzi hali ambayo itachangia maendeleo nchini.