Story by Hussein Mdune-
Mgombea wa kiti cha ubunge wa Jomvu Abdulhakim Ramadhan Kajembe amewataka wanasiasa kukoma kueneza siasa za chuki na ukabila.
Abdulhakim amesema siasa ya chuki na ukabila huenda zikachangia mgawanyiko wa kijamii huku akiwahimiza wakaazi wa eneo bunge hilo kuwa makini katika kufanya maamuzi ya kuwachagua viongozi na kuwaunga mkono viongozi wenye malengo ya maendeleo.
Mwanasiasa huyo amewahimiza vijana na wakaazi wa eneo bunge hilo na kaunti nzima ya Mombasa kujitenga na siasa za vurugu na kutokubali kutumiwa vibaya na wanasiasa.
Wakati uo huo amewashukuru wakaazi wa Jomvu kwa kuamini uongozi wake kutokana na utafiti wa kura ya maoni uliofanywa na Shirika la utafiti la wagombea wa nyadhfa mbalimbali za uongozi la Center for African Progress yaan CAP na kumuorodhesha kama kiongozi bora.
Kwa upande wake Afisa wa Shirika la Center for African Progress CAP Ochari Oyeyo amesema utafiti huo umefanyika kwa usawa na haki kwa umezingatia kauli za wakaazi wa eneo bunge la Jomvu.