Viongozi wa kidini kaunti ya Mombasa wamewaonya viongozi wa kisiasa nchini kukoma kuendeleza siasa za kuwagawanya wakenya kikabila.
Kulingana na Askofu wa kanisa la Ushindi baptist Joseph Maisha amesema kuwa hatua hii huenda ikasababisha taifa hili likakosa amani endapo tabia hiyo haitakomeshwa Mara moja.
Maisha aidha Amewataka viongozi kujitenga na siasa za uchaguzi wa Mwaka 2022 kwani amesema siasa hizo zinazidi kudidimiza uchumi wa taifa hili.
Haya hivyo amewataka viongozi wa kisiasa humu nchini kukoma kuingilia utendakazi wa rais Uhuru Kenyatta na badala yakushirikiana naye kuimarisha taifa hili.
Wakati uo huo amesema Taifa hili litakuwa na biashara nzuri na uchumi mzuri endapo viongozi watasaidia kikamilifu Bali sikutengane kisiasa.
Taarifa na Hussein Mdune.