Story by Hussein Mdune-
Mgombea wa kiti cha uwakilishi wadi ya Tsimba/Golini katika kaunti ya Kwale Suleiman Mrisa Mwajoto amewataka viongozi ambao wanawania wadhfa huo kuendeleza kampeni za amani.
Mwajoto ambaye anawania kiti hicho kupitia chama cha CPK amesema siasa ni sera na wala sio chuki hivyo basi akawataka viongozi wa kisiasa kuendeleza kampeni za kuwaunganisha wananchi ili wadumishe amani.
Mwanasiasa huyo amewatka vijana na Wanawake katika wadi hiyo kujitenga na siasa za vurugu na badala yake kufanya uchaguzi wa amani.
Hata hivyo ameahidi kuimarisha viwango vya biashara kwa wafanyibiashara wadogo wadogo katika wadi hiyo ili kuhakikisha wanajiendeleza kimaisha.