Story by Hussein Mdune–
Wagombea watano wa kiti cha uwakilishi wadi ya Samburu/Chengoni katika kaunti ya Kwale akiwemo Emmanuel Mbandi, Edward Dalu Chinyama, Emmanuel Mwayaya na Elias Tsimba wamehudhuria mdahalo wa kuwapiga msasa wanasiasa uliyoandaliwa na mashirika ya kijamii ya Sports Connect na Samburu Hands of Compassion
Akielezea jinsi atakavyoboresha sekta ya elimu katika wadi hiyo, mgombea wa kiti hicho kwa tiketi ya chama cha Kanu Emmanuel Mbandi ameahidi kuhakikisha watoto wanaotoka kwa familia zisizojiwezi wanapata elimu.
Naye mgombea wa kiti hicho kupitia chama cha ODM Emmanuel Mwayaya ameahidi kushukishwa kwa ushuru kwa wafanyibiashara wadogowadogo ili waendeleze biashara zao bila changamoto.
Kwa upande wake Edward Dalu Chinyama anayewania kiti hicho kwa chama cha UDA ameahidi kulitatua swala tata la uhaba wa maji katika wadi hiyo.
Hata hivyo Mwenyekiti wa shirika la kijamii la Samburu Hands of Compassion Berdson Nyawa Kalu amewarai vijana kujitenga na siasa za vurugu na badala yake wadumishe amani.
Wakati uo huo Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Sports Connect Athanus Mdoe amesema kuna haja ya viongozi kuangazia talanta za vijana katika sera zao.