Story by Hussein Mdune-
Mgombea huru wa kiti cha uwakilishi wadi wa Samburu/Chengoni katika kaunti ya Kwale Elisha Kalu Mwango amesema kuna haja ya jamii ya watu wanaoshi na mahitaji maalum kutambuliwa kama watu wengine.
Mwango amesema mlemavu yuko na haki sawa na mtu mwengine katika jamii na anastahili kunufaika na miradi yote inayotolewa kwa jamii.
Mwango ameahidi kuwajenga uwezo walemavu kupitia biashara na ajira ili kuhakikisha wanajikimu kimaisha na kuendeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika jamii.
Kwa upande wake Elias Tsimba ambaye ni mgombea huru wa kiti hicho ameahidi kuboresha talanta za vijana sawa na kubuni miradi mbalimbali ya ajira itakayohakikisha vijana wanakabiliana na changamoto zinazowasibu.