Viongozi wa kisiasa kaunti ya Mombasa wamezidi kuikosoa ripoti iliotolewa na shirika moja la utafiti nchini kuhusu viongozi wanaohusika katika sakata za ufisadi.
Wakiongozwa na mwanaharakati wa maswala ya kisiasa kaunti hio Abdi Daib viongozi hao wamesema kuwa ripoti hiyo haikua na msingi wowote badala yake ilitolewa kwa lengo la kuwagonganisha wananchi.
Daib ameitaka idara ya usalama nchini kuyachukulia hatua mashirika yanyoendeleza utafiti humu nchini kinyume cha sheria.
Taarifa na Hussein Mdune.