Wakaazi wa eneo la Magarini kaunti ya Kilifi wanaoendeleza mauaji ya wazee kwa tuhuma za uchawi wameonywa kukomesha uovu huu la sivyo wataandamwa na mkono wa sheria na kuadhibiwa vikali.
Afisa mkuu wa polisi eneo la Magarini Gerald Barasa amewataka wanaodai wazee hao ni wachawi kuripoti kwa idara husika badala ya kuchukua sheria mikononi mwao.
Barasa amesema kuwa kuwauwa wazee hao ni ukiukaji wa haki yao ya kuishi akisema wana haki kuishi kama wakenya wengine.
Afisa huyo wa polisi amedokeza kwamba idara ya usalama eneo hilo imeidhinisha mikakati kukomesha mauaji ya wazee ambao hushuhudiwa mara kwa mara.
Taarifa na Esther Mwagandi.