Idara ya usalama kaunti ya Kilifi imewataka wakaazi wanaoishi katika ardhi ya mradi wa upanuzi wa uwanja wa ndege wa Malindi na ambao tayari wamefidiwa kuodoka kwenye ardhi hiyo mara moja ama waondolewe kwa nguvu.
Akiongea huko Malindi wakati wa ukaguzi wa mradi huo kamishna kaunti ya kilifi Magu Mutindika amesema kuwa licha ya waliofidiwa kupewa miezi mitatu kuondoka eneo hilo,wakaazi hao wamepuuza agizo hilo.
Kauli ya Mutindika imeungwa mkono na meneja wa uwanja wa Ndege wa Malindi Mohamed Karama ambaye amesema kuwa serikali imetumia jumla ya shilingi milioni 418 kufidia takriban familia 120 katika awamu ya Kwanza.
Amesema kuwa ujenzi wa uwanja wa ndege wa Malindi bado unaendelea akisema kuwa tayari maeneo ya kuegesha Magari na ndege ndogo yamekamilika.