Picha kwa hisani –
Huenda wakaazi wa kaunti ya Kilifi ambao wamekuwa wakiishi kama maskota kwa miaka mingi sasa, wakakabidhiwa hati miliki za ardhi baada ya Wizara ya Ardhi nchini kuzindua mpango huo.
Katibu mkuu msimamizi katika Wizara hiyo Gideon Mung’aro, amesema Wizara hiyo katika awamu ya kwanza ya mpango huo ilitoa hati miliki laki moja kwa wakaazi wa Pwani na sasa inalenga kuanzisha awamu ya pili.
Akizungumza kule kaunti ya Kilfi, Mung’aro amesema mpango huo umeangazia kaunti zote za Pwani ambako suala la ardhi limekuwa donda sugu.
Wakati huo uo amedokeza kuwa serikali inaaendelea na mazungumzo na baadhi ya mabwenyenye walio na ardhi kubwa kubwa ili kuzinunua na kuzigawa kwa wakaazi.