Story by Janet Shume-
Idara ya usalama katika eneo bunge la Kinango kaunti ya Kwale imetoa tahadhari kwa wakaazi wa eneo hilo dhidi ya kutapeliwa na watu wanaodai kwamba watawasaidia kupata nafasi za kazi hususan ya ualimu.
Afisa mkuu wa polisi eneo hilo, Fredrick Ombaka amesema maafisa wa polisi wampokea ripoti ya visa hivyo kwamba kuna baadhi ya watu ambao wametapeliwa fedha zao kwa madai kwamba watapewa kazi na watu wasiojulikana na baadae kugundua kwamba wamelaghaiwa.
Ombaka amesema idara ya polisi itakabiliana kikamilifu na watu hao kwani ni kinyume na sheria kuendeleza utapeli humu nchini.
Wakati uo huo amesema idara ya usalama inaendeleza uchunguzi wa nambari za simu zilizotumika kutekeleza utapeli huo ili kuwakamata wahusika na kuwachukulia hatua kali za kisheria.