Story by Janet Shume-
Serikali ya kaunti ya Kwale imetoa onyo kali kwa wale wanaoendeleza uharibifu wa mabomba ya maji na kujiunganishia wenyewe kinyume cha sheria kwamba watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Gavana wa Kwale Fatuma Achani amesema kumeshuhudiwa ongezeko la visa hivyo vya ukataji mabomba ya maji kiholela akihoji kwamba hali hiyo imechangia kukithiri kwa uhaba wa maji katika maeneo mbalimbali ya kaunti hiyo.
Achani amesema hatua hizo zitahakikisha wakaazi wa kaunti ya Kwale wananufaika na huduma bora za maji huku akiwarai wakaazi kulinda raslimali za kaunti hiyo.
Kwa upande wake Kamishna wa kaunti hiyo Gideon Oyagi amewataka wakaazi kuripoti visa hivyo kwa maafisa wa usalama ili washukiwa wachukuliwe hatua kali za kisheria.