Mwakilishi wa Kike kaunti ya Taita Taveta Lydia Haika amewaonya watu wanaoendeleza dhulma za kijinsia katika kaunti hiyo, akisema watakabiliwa kisheria.
Haika amesema atahakikisha haki inapatikana kwa waathirika wa dhulma hizo hasa wanawake na watoto wadogo.
Akizunguzma na Wanahabari, Haika amesema watuhumiwa wanaotumia kigezo cha umaskini na kuwalaghai waathiriwa ili wazifuatilie mbali kesi za dhulma za kijinsia pia nao hawatasazwa.
Kiongozi huyo ameahidi kuzishughulikia kesi hizo ili kuhakikisha waathirika wanatapata haki kwa mujibu wa sheria.
Taarifa na Fatuma Rashid.