Story by Mwanaamina Fakii –
Waziri wa Utalii na biashara katika serikali ya kaunti ya Kwale Nassir Nyahi amesema imekuwa changamoto kwa kaunti hiyo kudhibiti biashara ya vileo harumu.
Akizungumza na Wanahabari, Nyahi amesema idadi kubwa ya wafanyibiashara wa vileo ambao wanauza pombe zisizo halali wamekuwa wakikwepa kulipa ushuru hali ambayo imechangia serikali hiyo kukosa kukusanya ushuru wa kutosha.
Nyahi hata hivyo amewataka wananchi kujitokeza na kuwaripoti kwa idara ya usalama wale wote wanaoendeleza biashara hiyo haramu ili wachukuliwe hatua.
Kwa upande wake Kamishna wa kaunti ya Kwale Gideon Oyugi amesema vitengo vyote vya usalama vitashirikiana na wadau mbalimbali katika juhudi za kudhibiti uuzaji wa pombe haramu.