Afisa Mkuu Mtendaji wa Bodi ya filamu nchini Ezekiel Mutua amewaonya watakaoendelea kuonyesha filamu ya Rafiki iliyopigwa marufuku na bodi hiyo kuwa watakabiliwa kisheria.
Mutua anasema japo idara ya Mahakama ilipeana fursa kwa filamu hiyo kuonyeshwa kwa mda wa siku 7 ili kuiwezesha kushiriki kwenye tuzo za Oscar Awards, sheria ni lazima izingatiwe kikamilifu.
Akizungumza mjini Mombasa, Mutua amesema bodi hiyo haitaruhusu filamu hiyo kuendelea kuonyeshwa hadi pale baadhi ya vipengele kwenye filamu hiyo vitakaporekebishwa.
Taarifa na Cyrus Ngonyo.