Story by Ali Chete-
Vijana katika kaunti ya Mombasa waonywa dhidi ya kubeba silaha katika mikutano ya kisiasa.
Kamanda mkuu wa polisi kaunti ya Mombasa Stephen Matu amesema ni hatia kwa mtu yeyote kubeba silaha ama bakora mikutano ya kisiasa, akihoji kwamba serikali hatakubali tabia hiyo.
Matu amewaonya vijana dhidi ya kutumika vibaya na wanasiasa, akisema yeyote atakaepatikana akivurugu mikutano ya kisiasa atachukuliwa hatua za kisheria huku akiwarai wananchi kudumisha amani.
Kauli ya Afisa huyo wa polisi imeungwa mkono na baadhi ya Wanaharakati wa kijamii wakiongozwa na Mkurugenzi mkuu wa vuguvugu la First Action Business Harriet Muganda waliosema hatua hiyo itaimarisha usalama kaunti hiyo.