Story by Hussein Mdune–
Mgombea mwenza wa kiti cha ugavana wa kaunti ya Kwale kwa tiketi ya chama cha UDA Chirema Kombo amewataka wakaazi wa Samburu/Chengoni kupiga kura kwa Amani
Akizungumza na Wanahabari baada ya kupiga kura katika kituo cha kupigia kura cha shule ya msingi ya Chanzoi, Kombo amewataka wananchi kutojihusisha na vurugu.
Kiongozi huyo amewataka viongozi kutowachochea wakaazi kuzua vurugu, akisema ni lazima wananchi wadumishe amani.
Hata hivyo ameitaka Tume ya IEBC kuhakikisha vifaa vinavyoendeleza zoezi la upigaji havikumbwi na changamoto.