Mkurugenzi wa idara ya hali ya anga kaunti ya Kwale Dominic Mbindio, amewahimiza wananchi kuwa mabalozi wa utunzaji wa Mazingira, ili kukabiliana na mabadiliko tabia nchi.
Akiongea na Mwanahabari wetu afisini mwake, Mbindyo amesema shughuli za binadamu zimechangia mabadiliko tabia nchi, na kusababisha mabadiliko ya ghafla katika mazingira.
Amedokeza kuwa ukataji wa miti na ongezeko la Viwanda mijini, ni chanzo kikuu cha uchafuzi wa Mazingira.
Mkugenzi huyo hata hivyo amewataka wakaazi wa Kwale kupanda miti kwa wingi ili kurudisha hali ya zamani ya anga, huku akielezea hofu yake kuwa ongezeko la uchafuzi wa Mazingira litakuwa na athari zaidi katika maisha ya binadamu.
Taarifa na Michael Otieno.