Wanamziki wa Bango eneo la Pwani wameshtumu vikali hatua ya Kamishna wa Kaunti ya Kilifi Magu Mutundika na Gavana wa kaunti hiyo Amason Kingi kupiga marufuku sherehe zote za usiku kwa madai kuwa zimechangia mimba za mapema kwa wasichana wenye umri mdogo.
Wakiongozwa na Joseph Ngala Katana maarufu “Mzee Ngala” wanamziki hao wamesema kuwa hatua hiyo inahujumu pakubwa kazi yao ikizingatiwa kuwa wengi wao wanategemea pakubwa kutumbuiza kwenye hafla hizo kupata mapato.
Akizungumza katika eneo la Frère Town wanamuziki hao wameitaka serikali ya kaunti ya kilifi kulitahmini kwa kina swala hilo na kubuni mbinu mwafaka ya kulikabili tatizo la mimba za mapema na wala sio kuwakandamiza.
Msikilize Mzee Ngala hapa.
Taarifa na Cyrus Ngonyo.