Katika juhudi ya kuwahamasha Wakenya kuzuru maeneo mbalimbali ya kitalii humu nchini wanamitindo kutoka kaunti ya Migori, Transnzoia, Mombasa na chuo kikuu cha Catholic University wamezuru fukwe za Diani.
Wakiongozwa na mwanamitindo kutoka kaunti ya Migori Edith Owido wanamitindo hao wamehimiza wananchi kuanza kuzuru mikahawa, fukwe za bahari na sehemu zingine za vivutio vya utalii nchini.
Kulingana na Edith hatua hiyo itaongeza mapato ya hoteli hivyo basi kuongeza nafasi ya hoteli kuajiri watu wengi zaidi humu nchini.
Edith amekiri kuwa kutegemewa kwa watalii kutoka nje pekee hakutoshi kustawisha sekat ya Utalii.
Taarifa na Salim Mwakazi.