Story by Ngombo Jeff-
Wakaazi wa kaunti ya Kilifi wametakiwa kusikiza na kutathmini kwa kina sera za wagombea wa nyadhfa mbalimbali za uongozi ili kuhakikisha wanachagua viongozi waadilifu
Afisa wa mipango katika Shirika la kutetea haki za kibinadamu la HURIA Betty Sidi, amesema midahalo ya wagombea wa nyadhfa za kisiasa ambayo imekuwa ikifanyika inalenga kuwapa wananchi ya kufahamu viongozi watakaojali maslahi yao.
Akizungumza mjini Malindi baada ya mdahalo wa wagombea wa kiti cha ubunge wa eneo hilo, Sidi amesisitiza haja ya wananchi kuwa makini wanapofanya maaamuzi ya kuwachagua viongozi wakati wa uchaguzi mkuu wa Agosti 9.
Kwa upande wake Mwakilishi wa jamii ya watu wanaoishi na ulemavu eneo la Malindi Mary Jumwa amesema kufanyika kwa midahalo hiyo kumewasaidia kuzitambua sera za wagombea wa nyadhfa mbalimbali huku akisema midahalo hiyo itawapa nafasi wananchi kuwauliza sera viongozi.