Picha kwa hisani –
Huku ulimwengu ukiadhimisha siku ya kimataifa ya waathiriwa wa kupotea katika hali tatanishi, Mashirika ya kutetea haki za kibinadamu kanda ya Pwani kwa ushirikiano na wakaazi wa kaunti ya Kwale wamefanya maandamano ya amani.
Maandamano yalianza katika maeneo ya Kona ya Musa kule Ukunda hadi katika afisa ya mkuu wa polisi eneo la Diani yanalenga kuishinikiza serikali kulinda haki za binaadamu dhidi ya mauaji yanayodaiwa kutelezwa na watu wanaoamini kuwa polisi.
Mashirika hayo yakiongozwa na lile la HUDA, Haki Afrika pamoja na Huria, chini ya Afisa wa Shirika la HUDA Kashi Jamein Wamesema kufikia sasa wamenakili visa zaidi ya 60 vya watu waliouwawa katika hali tatanishi.
Mtetezi huyo wa haki za kibiadamu amesisitiza kuwa zaidi ya watu 30 kwenye kaunti hiyo wameripotiwa kupotea.