Picha kwa hisani –
Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu kanda ya Pwani wamejitokeza na kuitaka Serikali ya kaunti ya Mombasa kufutilia mbali azma yake ya kuwaachisha kazi madaktari katika kaunti hiyo.
Wanaharakati hayo wakiongozwa na Mkurugenzi mkuu wa Shirika Haki Afrika Hussein Khalid wamesema hatua ya kuwafuta kazi madaktari hao haiwezi kusuluhisha hali tata inayoikumba sekta ya afya kaunti ya Mombasa.
Kulingana na Khalid, Wanaharakati hao wanaunga mkono kikamilifu mgomo huo kwani madaktari hao wanapigania kikamilifu haki zao na mazingira bora ya kufanyia kazi.
Wakati uo huo, amehimiza majadiliano ya kina kati ya Serikali ya kaunti hiyo na madaktari hao ili kuutanzua mgogoro huo unaoikumba sekta ya afya.
Kauli ya Khalid imejiri huku tayari Serikali ya kaunti ya Mombasa ikiwapiga kalamu madaktari 86 kwa kushiriki mgomo.