Story by Bakari Ali –
Wanaharakati wa kijamii katika kaunti ya Kilifi wamewaonya wanasiasa wa Kike dhidi ya kuendeleza siasa za chuki na za uchochezi.
Wakiongozwa na Mkurugenzi wa Shirika la Kilifi Mums Kibibi Ali, Wanaharakati hao wamesema hawatawaruhusu wanasiasa wa Kike katika kaunti hiyo kuendeleza siasa potofu miongoni mwa jamii.
Kibibi ameitaka serikali kuweka mikakati mwafaka ya kuwahamasisha wanawake kuhusu muongozo wa Katiba, akisema hatua hiyo itahakikisha wanawake wanafahamu haki zao.
Kwa upande wake, mkurugenzi wa shirika la Kilifi Social Justice Samuel Kazungu amesema mashirika ya kutetea haki za kibinadamu katika kaunti ya Kilifi yatashirikiana na wagombania mbalimbali wa Kike ili kuibuka na suluhu la matatizo wanayoyakumba.