Story by Mwanaamina Faki-
Shirika la kijamii linaloangazia masuala ya dhulma za kijinsia katika kaunti ya Kwale la Hijab Mentorship limesema wakaazi wa kaunti hiyo wanajitokeza kwa wingi katika kuripoti visa vya dhulma za kijinsia.
Msimamizi wa miradi katika shirika hilo Salama Majaliwa, amesema hatua hiyo imetokana na hamasa zinazotolewa kwa wakaazi kuhusu umuhimu wa kuripoti visa hivyo.
Kwa upande wake Fredrick Maneno aliye balozi wa kupambana na dhulma za kijinsia kaunti ya Kwale amesema iwapo wanaume watashirikishwa katika masuala ya dhulma za jinsia basi visa hivyo vitatokomezwa.