Story by Ali Chete –
Wanaharakati wa maswala ya kijamii na wale wa kimazingira wameitaka seikali ya kaunti ya Mombasa na Mamlaka ya mazingira nchini NEMA katika kaunti hiyo kuondoa jaa la taka lililoko katika makaburi ya Manyimbo eneo la Tudor.
Wakiongozwa na Mwenyekiti wa Tume ya Amani ya Kanisa katoliki jimbo la Mombasa Mary Nyaga amesema mahali hapo panastahili kupewa heshima maana ni mahali panapostiriwa miili ya watu huku akisisitiza haja ya jaa hilo kuondolewa
Mary amehoji kuwa kamati hiyo ikishirikiana na wanafunzi wa chuo kikuu cha ufundi cha Mombasa TUM waliandaa hamasisho la kufanya usafi wa mazingira huku akisema ukosefu wa kuheshimu ndio umechangia mahali hapo kuwa jaa la taka.
Kauli yake imeungwa mkono na Mwanaharakati John Pual Obonyo kutoka Shirika la Haki Yetu aliyeikosoa serikali ya Mombasa kwa kushindwa kutengeneza mahali maalum pa kutupa taka.