Story by: Mwahoka Mtsumi
Mkurugenzi mkuu wa Shirika la kutetea haki za kibinadamu la Haki Africa Hussein Khalid amesema japo taifa linashuhudia utovu wa usalama unaochangiwa na wahalifu ni lazima sheria izingatiwe.
Khalid amesema sheria zilizobuniwa nchini ni lazima zizingatiwa ndipo visa vya utovu wa usalama vitadhibitiwa nchini lakini sio haki kwa maafisa wa usalama kutumia nguvu kupita kiasi wakati wanapopambana na wahalifu.
Khalid amesema japo Wanaharakati wa kutetea haki za kibinadamu wanaunga mkono juhudi zote za kukabiliana na wahalifu nchini lakini ni lazima juhudi hizo zizingatie sheria.
Kwa upande wake Afisa wa Shirika la Amnesty International Zaina Kombo, anataka kushurutishwa kwa serikali kuchukua hatua za haraka za kuzisaidia familia kutafuta wapendwa wao waliopotea katika hali tatanishi humu nchini.