Story by Bakari Ali–
Wanaharakati wa kijamii katika kaunti ya Mombasa wamelalamikia kucheleweshwa kwa zoezi la upigaji kura katika baadhi ya vituo cha kupigia kura katika kaunti hiyo.
Wakiongozwa na Afisa wa maswala ya dharura wa Shirika la kutetea haki za binadamu la MUHURI Francis Auma wamesema kucheleweshwa kwa zoezi hilo huenda kukachangia mivutano ya kisiasa.
Auma amewalaumu maafisa wa tume ya IEBC katika kaunti ya Mombasa kwa kulemaza zoezi hilo la upigaji kura katika baadhi ya vituo vya kupigia kura vya eneo bunge la Mvita.
Wanaharakati hao wameshikilia kwamba ni lazima hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya maafisa hao kwani wameshindwa hata kuwaeleza wananchi sababu zilizochangia kucheleweshwa kwa zoezi hilo.