Story by Gabriel Mwaganjoni –
Muungano wa mashirika ya kijamii kanda ya Pwani umekashfu vikali mauaji ya watu wawili katika eneo la Likoni kaunti ya Mombasa .
Muungano huo ukiongozwa na Afisa wa maswala ya dharura wa Shirika la Haki Afrika Mathias Shipetta, wametaka maelezo zaidi kutoka kwa polisi kuhusu mauaji hayo.
Akiwahutubia Wanahabari katika hifadhi ya maiti ya hospitali kuu kanda ya Pwani ambako miili hiyo imefanyiwa upasuaji , Shipetta amesema mauaji hayo ni ukiukaji mkubwa wa sheria na haki.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa mashirika hayo kanda ya Pwani Simon Kazungu amekiri kuwa maafisa wa polisi katika eneo la Pwani wamekiuka pakubwa haki za kibinadamu.