Swala la wazee kuuwawa kwa tuhma za uchawi katika kaunti ya Kilifi limeonekana kuwa tata mno hali ambayo imewalazimu watetezi wa haki za kibinadamu kuimarisha hamasa kwa jamii kuhusu hali hiyo.
Mwenyekiti wa mashirika ya watetezi wa haki za kibinadamu kaunti ya Kilifi Simon Kazungu amesema licha ya kampeni kuidhinishwa, swala hilo limekuwa tata na visa vya mauaji ya wazee vikiendelea kushuhudiwa katika jamii.
Akizungumza katika kaunti ya Mombasa, Kazungu amesema ni sharti kila juhudi ziidhinishwe ili kuwalinda wakongwe ambao kwa sasa wanaishi kwa hofu.
Wakati uo huo, Mwanaharakati huyo wa haki za kibinadamu amesema tayari watetezi wa haki za kibinadamu wamezidisha hamasa mashinani ili kuikomesha hali hiyo.