Story by Gabriel Mwaganjoni –
Wakereketwa wa maswala ya kijamii kisiwani Amu wamedhihirisha wasiwasi wao kufuatia mirundiko ya taka inayoshuhudiwa katika eneo la Mkunguni Kisiwani humo.
Wakiongozwa na mkurugenzi mkuu wa Shirika la Lamu Justice Network Yunus Ahmed, wakereketwa hao wamesema hali hiyo ni ya kusikitisha na ni sharti mirundiko hiyo ya taka iondolewe.
Ahmed ameitaka Serikali ya kaunti ya Lamu kuliwajibikia swala hilo na kuhakikisha hakuna mirundiko ya taka Kisiwani Amu.
Wakati uo huo, amehoji kwamba Serikali ya kaunti ya Lamu ina uwezo wa kuwapatia akina mama na vijana kandarasi hiyo na kisha kuwalipa ujira unaostahili ili kudhibiti uvundo huo.