Story by Gabriel Mwaganjoni-
Swala la usalama katika eneo la Likoni kaunti ya Mombasa limezidi kuwa tata mno baada ya kubainika wazi kwamba maswala ya ushirikina yanahusishwa na uhalifu huo.
Kulingana na mtetezi wa haki za kibinadamu katika eneo hilo Fahad Changi, swala hilo limechukua mkondo tofauti huku magenge ya vijana wadogo yakisemekana kugangwa kabla ya kutekeleza uvamizi.
Changi amedai kwamba mbali na swala hilo la ushirikina na kuwatia hofu wenyeji vile vile limepelekea vita dhidi ya uhalifu katika eneo hilo la Likoni.
Hata hivyo, mtetezi huyo wa haki za kibinadamu kanda ya Pwani anashinikiza jitihada za pamoja katika kudhibiti msukosuko wa kiusalama unaoshuhudiwa katika eneo la Likoni.