Story by Gabriel Mwaganjoni –
Waraibu wa dawa za kulevya wanaotiwa nguvuni na kufikishwa mahakamani hunyimwa haki kutokana na hali yao ya kutoweza kujieleza vyema ili kupata msaada wa kiafya.
Afisa wa maswala ya nyanjani wa Shirika la kupambana na uraibu wa dawa za kulevya la Reachout Centre Trust Pili Saria amesema hali hiyo imelilazimu Shirika hilo kushirikiana moja kwa moja na idara ya mahakama nchini ili kuzitatua changamoto hizo.
Akizungumza katika kaunti ya Mombasa wakati wa mkao na Majaji na mahakimu sawa na Maafisa wengine wa idara ya mahakama, Saria amesema Shirika hilo limewekeza hamasa ili kuhakikisha maafisa wa idara ya mahakama wana ufahamu kuhusu afya za waraibu hao.
Wakati uo huo, Afisa huyo wa maswala ya haki na sheria katika Shirika hilo la hilo amekariri kwamba juhudi hizo zimezaa matunda.