Story by Gabriel Mwaganjoni –
Shirika la kutetea haki za kibinadamu la Haki Afrika limeshikilia kwamba swala la watu kupotezwa na kuuwawa katika hali tata mikononi mwa maafisa wa polisi bado ni tata katika eneo la Pwani.
Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Hussein Khalid amesema ni sharti hali hiyo ikomeshwe, akishikilia kuwa wakereketwa wa haki za kibinadamu wamewekeza kila mbinu katika kuidhibti hali hiyo.
Kulingana na Khalid, ni sharti vitengo vya usalama vitekeleze majukumu yao kwa kuzingatia sheria na haki za kibinadamu.
Khalid vile vile amefichua kwamba jamii imekuwa ikiwaandama washukiwa na kuwauwa hali ambayo huenda ikapelekea watu wasiyokuwa na hatia kupoteza maisha.